Masharti ya Huduma
Kwa kutumia website au mfumo wa Ngosha Multimedia, unakubaliana na masharti haya ya matumizi ya huduma.
Matumizi ya akaunti
Taarifa utakazoweka wakati wa usajili zinapaswa kuwa sahihi na unawajibika kulinda nenosiri, OTP na access ya akaunti yako.
Usimpe mtu mwingine access ya akaunti kwa namna inayoweza kuhatarisha data ya biashara yako au ya wateja wako.
Matumizi yanayokubalika
- Usitumie huduma kwa shughuli haramu, udanganyifu, spam au kuvamia mifumo ya wengine.
- Usipakie code, faili au maudhui yenye malware, copyright ya mtu mwingine bila ruhusa, au taarifa zinazokiuka faragha.
- Usijaribu kuzuia, kuharibu au kupita ulinzi wa technical wa huduma.
Trial, malipo na mipango
Baadhi ya mifumo ina trial au mpango wa bure na mipango ya kulipia. Bei, limits na features huonyeshwa kwenye landing page husika na zinaweza kubadilika kwa taarifa ya mapema.
Malipo ya huduma zilizolipiwa hayatoi ruhusa ya kutumia akaunti ya mtu mwingine au kuendesha matumizi yanayokiuka masharti haya.
Upatikanaji wa huduma
Tunajitahidi kuweka huduma zipatikane kwa uhakika, lakini maintenance, matatizo ya mtandao, watoa huduma wa nje au matukio yasiyotarajiwa yanaweza kusababisha muda mfupi wa kutopatikana.
Mawasiliano
Kwa msaada au maswali kuhusu masharti, wasiliana nasi kupitia info@ngosha.com au WhatsApp +255 754 644 199.