Sera ya Faragha
Tunaeleza hapa namna Ngosha Multimedia inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako unapokuwa unatumia huduma zetu.
Taarifa tunazokusanya
Tunaweza kupokea jina, namba ya simu, barua pepe, taarifa za biashara na taarifa utakazoweka ndani ya mfumo unaotumia.
Kwa zana zinazofanya kazi kwenye kifaa chako, kama Kilimo, baadhi ya taarifa zinaweza kuhifadhiwa kwenye browser au kifaa chako badala ya kutumwa kwenye server.
Tunatumia taarifa kwa nini?
- Kukupa na kuboresha huduma ulizoomba.
- Kukusaidia kupitia WhatsApp, simu au barua pepe.
- Kukulinda dhidi ya matumizi mabaya, spam na majaribio ya kuvamia.
- Kukutumia taarifa za bidhaa ikiwa umejiunga na newsletter.
Kushirikisha taarifa
Hatuuzi taarifa zako binafsi. Tunaweza kutumia watoa huduma wa kiufundi, malipo au mawasiliano pale inapohitajika kutoa huduma, kwa masharti ya usalama na usiri.
Haki zako
Unaweza kuomba kujua taarifa tulizonazo, kusahihisha taarifa zisizo sahihi, kuomba kufuta taarifa pale sheria na mahitaji ya huduma yanaporuhusu, au kujiondoa kwenye mawasiliano ya matangazo.
Mawasiliano
Kwa maswali kuhusu faragha, wasiliana nasi kupitia info@ngosha.com au WhatsApp +255 754 644 199. Sera hii inaweza kusasishwa tunapoboresha huduma zetu.