Ngosha Toolbox 2026 ni programu kuu na kamili ya kuweka kompyuta yako ya Windows katika afya bora, kusafisha takataka zote za mfumo (Junk files), kuboost kumbukumbu ya RAM, kudhibiti programu zinazowaka na Windows, na kupanga mafaili kiotomatiki. Toleo hili jipya la v1.4.0 limejengwa kwa Python na C++ kwa ufanisi wa juu bila faili taka — ni jepesi, imara na linafanya kazi 100% bila intaneti.
Ufuatiliaji wa Afya ya Kompyuta (PC Health)
Ona matumizi halisi ya CPU, RAM, afya ya diski zote (C:, D:), taarifa za mfumo (specs), na muda ambao kompyuta imekuwa hewani (uptime).
Usafi wa Takataka (System Cleaner)
Safisha mafaili ya muda (Windows Temp, Prefetch), browser caches (Chrome, Edge, Firefox), crash dumps na kumbukumbu zilizokwama.
Kuboosti Kumbukumbu ya RAM (RAM Booster)
Punguza msongamano wa RAM kwa mbofyo mmoja tu (Trim working sets) ili kompyuta yako ifanye kazi kwa kasi bila kuizima.
Meneja wa Startup (Startup Manager)
Kagua na dhibiti programu zote zinazojifungua zenyewe wakati Windows inawaka ili kuongeza kasi ya kuwaka kwa kompyuta.
Kusafisha Nakala za Mafaili (Duplicate Cleaner)
Gundua mafaili yaliyojirudia kwa uhakiki wa SHA-256 hash. Hufuta salama kwa kupeleka kwenye Recycle Bin ili usipoteze data.
Mpangaji Mahiri wa Folda (Smart File Organizer)
Panga maelfu ya mafaili ndani ya sekunde kwa aina zake (Nyaraka, Picha, Video, Muziki) au kwa tarehe, ukiwa na uwezo wa Undo.
Windows 10 & 11 (64-bit)
Inajumuisha Setup EXE, Portable & Mwongozo
Hakuna Matangazo wala Ufuatiliaji
Ngosha PDF 2026 ni programu kamili ya kisasa ya PDF ya Windows. Imeundwa kusoma nyaraka kwa ubora wa juu wa HD, kuhariri PDF moja kwa moja (In-place save Ctrl+S), kugonga mihuri rasmi ya nyaraka (Approved, Paid, Confidential, n.k.), kutoa maandishi kwa OCR ya Kiswahili na Kiingereza bila intaneti, kuunganisha na kupanga kurasa, na kujiweka kuwa Default PDF Viewer ya kompyuta yako.
HD PDF Reader & Dark/Light Mode
Usomaji safi sana wenye zoom kuanzia 25% hadi 400%, utafutaji wa haraka wa maneno, na badiliko la rangi ya giza/mchana.
Uhariri wa Moja kwa Moja (In-Place Edit)
Weka maandishi mapya juu ya PDF, funika makosa (Whiteout mask), angazia (Highlight), na hifadhi moja kwa moja kwenye faili lile lile kwa Ctrl+S.
Mihuri Rasmi ya Nyaraka (Document Stamps)
Gonga mihuri ya Approved, Received, Paid, Confidential, au unda Muhuri Maalum wenye jina la ofisi, tarehe na jina la afisa muidhinishaji.
OCR ya Kiswahili na Kiingereza (100% Offline)
Badilisha nyaraka zilizoskaniwa au picha za kurasa kuwa maandishi yanayoweza kunakiliwa na kutafutwa bila kuhitaji bando wala wingu.
Unganisha, Tenga & Panga Kurasa
Unganisha PDF nyingi kuwa faili moja, tenga kurasa, zungusha (Rotate), au panga namba mpya za kurasa kwa mpangilio unaotaka.
Nywila & Ulinzi wa AES (Encryption)
Funga nyaraka zako nyeti kwa nywila zenye usimbaji wa kiwango cha benki (128/256-bit AES Encryption) na uondoe nywila pale inapohitajika.
Windows 10 & 11
Default Viewer Ready
Inajumuisha Setup EXE, Portable & Mwongozo
Ngosha Defender ni zana nyepesi ya ziada ya Windows iliyobuniwa kulinda kompyuta dhidi ya virusi, malware na mafaili hatarishi yanayosambazwa kupitia flash drive (USB) na mafaili yaliyopakuliwa. Inafanya kazi bega kwa bega na Microsoft Defender bila kulemea mfumo wala kula nguvu za CPU.
Ugunduzi wa Kiotomatiki wa USB (Auto-Detect)
Inagundua mara moja flash mpya inapochomekwa na kukuuliza kabla ya kuikagua. Haianzi kamwe kusoma bila idhini yako ya wazi.
Uchambuzi wa Kiakili (Smart Heuristic Detection)
Hutambua mara moja mafaili yanayojifanya nyaraka kwa kutumia majina ya uwongo (mfano: ripoti.pdf.exe, invoice.xlsx.vbs, au picha.jpg.scr).
Karantini Salama (Fail-Safe Quarantine)
Huhamisha mafaili yenye mashaka hadi kwenye karantini iliyotengwa kwa uhakiki wa alama ya SHA-256 kabla na baada ya kuhamisha, bila kufuta faili kizembe.
Nyepesi na Kimya (Lightweight & Zero Lag)
Hakuna michakato mizito ya chinichini. Inafanya kazi tu unapoihitaji (On-demand) na hutumia rasilimali ndogo sana za kompyuta.
Windows 10 & 11
100% Offline & Zero Telemetry
NgoshaOffice Writer ni programu ya kisasa ya uandishi na uhariri wa nyaraka za kiofisi iliyoundwa kwa ajili ya kompyuta za Windows. Inakupa uwezo wa kuandika, kuhariri, na kuumbiza nyaraka katika miundo ya DOCX, RTF na TXT, pamoja na uchapishaji wa kurasa halisi (Print layout), uokoaji wa kazi kiotomatiki (Atomic recovery), na uwezo wa kutoa PDF zenye ubora wa juu.
Usaidizi Kamili wa DOCX & RTF
Fungua, hariri na hifadhi nyaraka za Microsoft Word bila kupoteza mitindo, majedwali, picha, au viungo vya mtandao (hyperlinks).
Mwonekano Halisi wa Kurasa (Paginated Print Preview)
Ona jinsi nyaraka zako zitakavyoonekana zikichapishwa kwenye karatasi za A4 kabla ya kuprint au kutoa PDF.
Utoaji wa PDF wa Ubora wa Juu (PDF Export)
Toa faili safi za PDF zenye vichwa vya juu (headers), chini (footers), na namba za kurasa kwa mpangilio sahihi wa kitaaluma.
Uokoaji wa Kazi Kiotomatiki (Atomic Snapshots)
Inahifadhi nakala salama za kila hatua unayoandika ili kuzuia upotevu wa taarifa hata kama umeme utakatika au kompyuta ikizimika ghafla.
Windows 10 & 11 (64-bit)
Native WPF Architecture
100% Offline • Sifuri AI